Tuesday, April 23, 2013

***NI ALEX NA MISOJI***

------------------***------------------

...23"Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. 24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja." Mwanzo 2:23-24

 

Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Alex Alphonce na Bi. Missoji Ngassa. Kwa neema za Mungu na fadhili zake ndio msaada mkuu kwa wawili hawa kuweza kufunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT Usharika wa Majengo Kihonda Jumamosi ya tarehe 13 mwezi April. 

 

"Saa zingine maneno hunitoka bila mpango, saa zingine, ulimi hauoni ukweli wa moyo, saa zingine, nikiwa juu sioni chini nikiwa chini nataka tuwe juuuuu ..." Alex akimwimbia mpenzi wake kutoka moyoni ndani na karibu kabisa ya bwawa la kuogelea Morogoro Hotel.

 

Alex, akijisafi tayari kabisa kwa shuguli. 

 

 

Aaachechecheee, misoji ndani ya saloon 

 Mr. & Mrs. Alex pamoja na wapambe wao Mr. & Mrs. John nje ya kanisa la KKKT Usharika wa Majengo.

Edwin Berbakat, hahahaaa Blogger mwenyewe nikiwa dereva wa maharusi siku hiyo. Hapa nilikuwa namsubiri Bibi harusi atoke saloon taya kumpeleka kanisani.

 Aaaaaah! kunanini tena bhana,, hapa tayari ilikwisha halalishwa mambo sasa ni hadharani na abiria chunga mzigo wako hii ni Couple mpya kabisaaa ulimwenguni ni Mr. & Mrs. Alex Alphonce.

 

Ryoba baba, mdau mkubwa sana na organizer wa matarumbeta pamoja na usafiri. Hakika jamaa anaweza ali_pray part yake ipasavyo. 

Kwa tabasamu la furaha na bashasha nyuso zaongea.

 "Ngoja nikutengeneze mamii" Wadau kwa mbaali wakifuatilia tukio na pozi za Edwin Berbakat kwa maalusi.

 Baada ya kumaliza shughuli za kufunga ndoa kanisani, ilifuatiwa na maandamano ambayo yalitufikisha katikati ya mji wa Morogoro na kuelekea moja kwa moja Morogoro Hotel kwa ajili ya kupata picha na mapumziko kidogo kabla ya kuelekea ukumbini.

 

Chezea ndoa wewe, wenye wivu wajipambe na wao waolewe (Sio mimi maneno ya MC Rama Kombo hayo) 

 

Hakika wamependeza sana hawa wapendwa.

Pozi na Edwin Berbakat.

Classmates wa ukweli hao...

Edwin Berbakat & Baba Lupi pamoja na maharusi wetu. Sisi tulikuwa moja ya wadau wakubwa kabisa kwanza staff pamoja na Bwana Harusi pia ni wadau wa usafiri siku ya tukio. 

Maharusi ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wapambe wao wakijivinjari katika mazingira bora kabisa ndani ya washika dau wakubwa kabisa wa location ya picha za harusi mkoani Morogoro ambao ni Morogoro Hotel. Ukifika mahali hapa hubuguziwi fanya kila uonalo jema kutenda hata kama usiponunua maji bado kwa ukarimu wao watakuachia ufurahie hali ya hewa safi na mazingira tulivu.

Alex & Misoji 

Hakika alipendeza

 Baada ya ya muda kupita tulielekea moja kwa moja mpaka ukumbini maeneo ya Ipo Ipo ya Mazimbu ukumbi wa Double M Karutta.

Mawifi utawataka hapa ni Mirimey na Ericey

Kama kawaida huwa hawakosekani mawifi, hapa ni Salamey na Jasmey 

Chezea Nadhey wewe 

Tulifungua musiki nauma hii.

Wadau mbali mbali walikuwepo hawa ni office dadaz wa Bwana Harusi


Napenda kumshukuru Mungu kwa ajili yao, kwa kuwawezesha kufanikisha malengo yao waliojiwekea nafsini mwao na kutimiza haja ya mioyo yao.

Kama Blogger; nawatakia mafanikio mema na Mungu awabariki sana katika maisha yenu mapya kabisa ya ndoa. 

Amina.