OFFICIALLY RELEASE OF MY NEW SONG #HABARI NJEMA**
Tarehe 31/01/2013 ni siku maalumu nilipoachilia kwa hewa wimbo wangu #HABARI NJEMA** na kila mwenye masikio aliyetapenda kuusikiliza aliusikia na aliyependa kuumiliki alimiliki. Niliutuma kwa wapendwa wangu kupitia kwenye akaunti yangu ya facebook www.facebook.com/eydwinshillah. Pia kwa sasa unaweza kuupata kupitia hulk share ya akaunti yangu www.hulkshare.com/shillah.
Nakupa nafasi ya upendeleo mpendwa katika Bwana wangu Yesu Kristo kujua mashahiri yote yaliyopo kwa song hili.
WIMBO: #Habari njema
MTUNZI na RAPA: Shillah
ALIYESHIRIKISHWA UIMBAJI: Lenny
ALIYESHIRIKISHWA UIMBAJI: Lenny
Kiitikio// Ameimba Lenny
Ni habari njema kwako sikia a a ah ah aaa!!
Yesu mwema anarudi,
Amekwenda kuandaa makao oo oh oh ooo!!
Yesu mwema anarudi,, aaaa aha aa!!
Ubeti 1// Umeimbwa na Shillah
Ni habari njema kwako
Habari za mashiko
Zenye kuleta mvuto
We ndugu tega sikio
kuzaliwa kwake Yesu
Kulileta pambazuko
Dunia ilikuwa tupu
Ikapata pumziko
Bikira,
Alishika mimba bila mume kuhusika
Naye Yesu akazaliwa
Kazi ya Mungu akajitwika
Maisha yakasonga
Akazidi tu kukua
Ki umri kihekima
Wakapata tu kumjua
Wanafunzi akachagua
Apate ambatana nao
Huduma anayoitoa
Ipate wafikia wao
Magonjwa yaliwatesa
Naye akaponya miili yao
Mapepo yaliwatoka
Yakawaacha huru wao
Wale wote walompokea
Walifanywa wana wa Mungu
Na kwake wakasogea
Wakaacha na miungu
Wapo, walomkimbia
Kusema si mwana wa Mungu
Kazi zake wakachukia
Wakasambaza majungu
Wakamteka, wakampiga
Usaliti alifanya Yuda
Wakamtesa wakampinga
Afunguliwe baraba
Eloi eloi
Ramasaba kitani
Mungu wangu Mungu wangu
Mbona umeniacha mimi
Wakamuweka msalabani
Yesu akafa abadani
Wakamshusha kaburini
Wasijue atarudi lini
Kafufuka yuko hai
Akapaa kama tai
Kaibiwa wakadai
Atarudi ba_dae.
Kiitikio// Ameimba Lenny
Ni habari njema kwako sikia a a ah ah aaa!!
Yesu mwema anarudi,
Amekwenda kuandaa makao oo oh oh ooo!!
Yesu mwema anarudi,, aaaa aha aa!!
Ubeti 2// Umeimbwa na Shillah
Atashuka na mawingu
Kila jicho litamuona
Na kila mwenye pumzi
Atasema Yesu ni Bwana
Anakuja kuhukumu
Walewote walomkana
Na Neno litasimama
Manabii walilonena
Amekwenda andaa makao
Juu kwa mbingu ndio kwao
Atachuku_wamfahao
Ili akaishi nao
Tena,
Hao ndio watarithi huo ufalme
Usioharibika udumuo
Watamiriki na ngome
Kazi hiyo,
Itakuwa ndo mwishowe
Vitabaki vilio,
Kwenye moto wa milele
Na hapo ndipo
Ndugu yangu utajuta
Utasema bora ningelijua
Ningelitubu kabisa
Tubu,
Tubu sasa angali neema bado ipo
Jumuika jumuiko
Siku hiyo tuwe huko
Ndugu,
Never never never be like shetani
Never give up
Never stay like godauni
Chunga chunga
Njia zako unazopitan
Hakikishan
Ziwe zimethibitishwan
Mungu wetu
Wala hapendezwi hata
Wanapokufan
Watu watenda mabayan
Bali waziache
Njia zao mbaya
Watapatwa na busara
Hawataona tena haya haya
Mmesikia
Yale niliyo yasema
Na kama tuko pamoja
Watu wote sema sawa sawa.
Daraja// Ameimba Lenny
Hii ndio habari njema kwako
Basi kaa tayari fanya mabadiliko
Haijulikani siku wala saa
Yesu atakayo kuja
Haijulikani siku wala saa
Muda umeshakwishaaa,, aaaah!
Kiitikio// Kimeimbwa na Lenny
Ni habari njema kwako sikia a a ah ah aaa!!
Yesu mwema anarudi,
Amekwenda kuandaa makao oo oh oh ooo!!
Yesu mwema anarudi,, aaaa aha aa!!
***MWISHO WA WIMBO***