Friday, January 11, 2013

Edwin Shilla (Shillah): Mwanamuziki wa Injili wenye maadhi ya Hip Hop!

Muziki wa Injili wenye maadhi ya hip hop mara nyingi umekuwa haukubaliki makanisani kwa asilimia kubwa. "Watumishi wengi wa Mungu wamekuwa hawaruhusu saana kupigwa hip hop (Gospel Hip Hop Music) makanisani wakizani kuwa ni muziki wa vijana na ni wa kihuni bila kufikiri yakuwa ni aina tu ya muziki kama ilivyo mingine.

 

Lakini wameshindwa kujiuliza kuwa mbona wengine wanapiga maadhi ya sebene, taarabu,R&B je, watasemaje kuwa hip hop ni uhuni?" anauliza Shillah. Pia anasema kwenye Biblia neno la Mungu halikuweka bayana ni aina gani ya muziki ambao ni rasmi utumike katika kumwabudu au kumsifu Mungu zaidi tu ya kuambiwa tumsifu Mungu kwa nyimbo,vinanda, vinubi matari na kucheza.

 

Hip Hop ni muziki wa kimarekani wenye nia thabiti ya kupeleka ujumbe mahali husika bila kuogopa wala kuhofia hadhira. Na unatumika mahali popote iwe kwenye burudani mbalimbali za kijamii, kidini, hafra za kiserikali n.k. Shillah anaendelea kusema "Uhuni ni tabia ya mtu lakini si muziki. Muziki wowote unaweza ukatumika kufikisha ujumbe lakini inategemea ujumbe wa aina gani ndio maana taarabu mara kadhaa hutumika kufikisha ujumbe wa mipasho, kuonyana na kutambiana, wakati sebene ni aina ya muziki kutoka Congo na uchezaji wake mara nyingi ni hatari sana kama ilivyo kwa taarabu lakini nao pia unatumika makanisani" anaendelea "Watu hucheza na kufurahi sana katika kusifu ukuu wa Mungu hasa sebene na ndio maana mimi pia kwa sababu nimelenga hasa vijana wenzangu hata na wazee kumrudia/kumpokea/kumkiri Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi katika maisha yao  ambao ni tegemeo kubwa katika taifa lolote lile iwe kijamii, kiuchumi, maendeleo, n.k." 

  anasema Edwin shilla (Shillah). Hivi sasa amerekodi nyimbo tatu ambazo wa kwanza unaitwa #Mungu ulinipenda kwanza, wa pili #Bwana Yesu ahsante na wa tatu ambao unatoka hivi karibuni unaitwa #Habari njema kwako ambazo zote amezifanya katika studio mbili tofauti hapa mkoani Morogoro ambazo ni Uptown music chini yake producer King Niver na nyingine ni Touch music kwenye uangalizi wa producer Meck Touch zenye maskani yake maeneo ya Ipo Ipo Mazimbu Mkoani hapa. Shillah anasema kuwa malengo yake ni kuhahikisha muziki wa aina hii unakuwa na kueleweka kuwa ni muziki kama ilivyo miziki mingine. Anaendelea kusema kuwa yeye pamoja na waimbaji wengine kama preacher Gazuko, Dp Deogras, Sir Alex Mbezi, Rungu la Yesu peke yao hawawezi kufanya muziki huu kuwa juu kama ilivyo mingine na kwa sababu hii ni huduma kama ilivyo huduma nyingine basi ni vyema wadau mbalimbali wakajitokeza kuusapoti muziki huu. 

Pamoja na hayo pia Shillah ni mfanyakazi mwajiriwa wa serikali ambaye ni Mkutubi (Librarian) kupitia Chuo kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) Campus ya Solomon Mahlangu Mazimbu mkoani Morogoro.

Yupo tayari kwa miariko kwenye matamasha mbali mabali, makanisani na hata katika mikutano ya Injili. Ukitaka kuwasiliana naye mtafute katika akaunti yake ya facebook na mfesibukike kupitia www.facebook.com/edwinshilla na kama utapenda aidha kupiga na kusikiliza (play) au kupakuwa (download) muziki wake pia tembelea akaunti yake nyingine ya facebook ambayo ni www.facebook.com/eddieshillah unachotakiwa kufanya ni ku-LIKE Page na kuanza kusafu. Pia waweza kumpata kupitia simu yake ya kiganjani ambayo ni +255712 247 560.

"Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu."  Mithali 1:7